Saturday 6 March 2010

Historia fupi ya Muziki wa Dansi.

Huwezi kuzungumzia muziki wa dansi nchini Tanzania bila ya kutaja majina mashughuli katika fani hiyo hapa nchini, kama vile Muhiddin Maalim (Gurumo), Hassani Bitchuka, Abel Balthazar, Nguza Mbangu, Mbaraka mWinyishehe, Saidi Mabera na Ndala Kasheba.

Majina hayo ni baadhi tu, ila wapo wengi ambao wametamba ipasavyo katika anga za muziki wa dansi, miongoni mwao wapo hai mpaka leo na baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.

Kwa mijibu wa historia Muziki wa dansi ni muziki asili yake ni kutoka nchini Tanzania. Ulianzishwa katika mji wa Dar es Salaam kunako miaka ya 1930, tangu ulipoanazishwa ulikuwa unapendwa hadi hii leo kuna baadhi ya watu hawawezi kuukosa.

Muziki wa dansi unatokana na muziki wa soukous kutoka Kongo-Kinshasa (au "rumba ya kikongo") na tokea hapo mwanzo ulipoanzishwa ukiitwa "rumba ya Tanzania", muziki wa dansi umekuwa ukiimbwa kwa lugha fasaha ya Kiswahili, muziki huu pia unaweza uita "swahili jazz" kwa lugha ya Kiingereza.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya mtandao Muziki wa dansi ulianzishwa kunako miaka ya 1920-1930, ukiwa na mandhari ya muziki wa "soukous" kutoka Kongo-Kinshasa, ambapo ulikuwa ukipendwa kote Afrika ya Mashariki.
Tokea hapo bendi mbalimbali zilianzidhwa na zilianza kubuni mitindo tofauti ya uimbaji , upigaji na uchezaji, kwa mfano Dar es Salaam Jazz Band, Morogoro Jazz na Tabora Jazz.
Baada ya uhuru wa Tanzania, bendi nyingi za muziki wa dansi zilitegemea ofisi au vyama. Kwa mfano, NUTA Jazz Band ilikuwa bendi bayana na ilitegemea Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania ("National Union of Tanzania", NUTA, kwa Kiingereza).
Kunako miaka ya 1960-1980 muziki wa dansi uliendelea kwa ajili ya bendi bayana kama Orchestra Safari Sound, Orchestra Maquis Original, International Orchestra Safari Sound, DCC Mlimani Park Orchestra na Vijana Jazz.
Bendi nyingi za muziki wa dansi zilikuwa zikifanya show mbalmbali kila usiku, katika vilabu, mahoteli na kadhalika, na wanamuziki walipokezana. Kwa mfano Morogoro Jazz ilicharaza katika hoteli ya "Morogoro Hotel" ya Morogoro. Pia wanamuziki walikuwa wakifanyakazi kwa kulipwa, na bendi ilikuwa imikimiliki vyombo vya muziki. Wanamuziki mashuuri walibadili bendi mara nyingi, hata kuchuma zaidi na hatimaye kuanzilisha bendi zao. Kwa mfano Muhiddin Maalin na Hassani Bitchuka walicharaza katika mabendi mengi.
Kila bendi huwa na mtindo unatambulikana, na mwanamuziki hujikaribisha kwa mtindo wa bendi yao baada ya kuajiriwa. Kwa kawaida jina la mtindo larejea gungu, kwa mfano ogelea piga mbizi ya Orchestra Maquis Original. Wasanii wengine walijulikana kwa sababu huweza kuunda mitindo vizuri.
Kwa kawaida, nyimbo za muziki wa dansi huanza polepole kusisitiza maneno, kasha muimbaji huongeza vionjo hatua kwa hatua na hukuwa haraka (kipande hiki huiitwa chemko), na ngoma na magitaa huongeza kwa sauti.
Katika kitu chochote ushindani ni lazima ambapo kuna kuwa na lengo moja kubwa zaidi ni kufanya kitu kivutie na kupendendwa zaidi na watu, hivyo hivyo Ushindani upo baina ya bendi zamuziki, Kwa mfano, Orchestra Maquis Original ilikuwa ikishindana na Orchestra Safari Sound (kunako miaka ya 1970-1980) na baadaye International Orchestra Safari Sound kushindana na Mlimani Park. Pamoja na hayo pia huwa na sherehe mbalimbali za muziki wa dansi ambapo mara nyingine hufanywa kama shindano.
Kwa kipindi hiki tulichonacho, katika dunia ya utandawazi muziki unaendelea kukua na mitindo ya aina mbalimbali inaibuka, tunashuhudia vijana wengi wanaingia katika fani hii, ila pamoja na hayo yote bado muziki wa dannsi upo katika chati na wasanii wakongwe kama Maalimu Gurumo wanaendelea kutamba.

2 comments: