Sunday, 7 March 2010
Mbaraka Mwinshehe akimvisha mke wake, Amney Shadad, pete ya ndoa. Hiyo ilikuwa tarehe 17/3/1972 mjini Morogoro.
Mbaraka alianza kujitengenezea jina kwenye medani ya muziki wakati alipokuwa mmojawapo ya wanamuziki waliokuwa wanaunda bendi maarufu ya Morogoro Jazz kati ya mwaka 1964 mpaka 1973. Baadaye ndipo alipoanzisha bendi yake mwenyewe iliyojulikana kama Super Volcano mwaka 1973. Alidumu na kutamba na Super Volcano mpaka mauti ilipomfika miaka sita baadaye. Kuimba alijifunza kutoka kwa Salum Abdullah, mwanzilishi wa Morogoro Jazz ambaye baadaye alijiengua na kwenda kuunda Cuban Marimba Band.Picha kwa hisan ya BONGO Cerebrity.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment