Friday 12 February 2010

Sakata la rushwa kwa Jerry Muro...

Jerri Muro si jina geni miongoni mwa watanzania wengi hasa wale wanaopenda kufuatilia vipindi mbalimbali vya Televission.

Ni miongoni wa waandishi chipukizi wanaochipukia na kukua kwa kasi katika tasnia ya uandishi wa habari hapa nchini.

Jina hili lilianza kung’aa mapema mwaka jana, ambapo kupitia kipindi cha RIPOTI maalumu kilichokua kikirushwa na kituo cha television cha ITV, ambapo alikuwa akiripoti habari za uchunguzi hasa kuhusiana na suala zima la rushwa.

Kwa mara ya kwanza kipindi chake kurushwa kilikuwa kinahusu masuala ya rushwa katika jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani, ambapo alionyesha baadhi ya askari hao wakipokea rushwa kutoka kwa madereva mbalimbali a gari za mizigo na hata zile za abiria.

Hivi karibuni mwandishi hiyo wa habari alipata mkasa wa yeye mwenyewe kutuhumiwa kuomba rushwa kutoka kwa aliekuwa mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.

Muro, mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji (TBC) na ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, anashikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi ambayo imeeleza kuwa habari zaidi kuhusu mkasa wake zitatolewa leo.

Habari za kupambana na kero ya rushwa na ufisadi jana zilimwingiza mwandishi huyo mikononi mwa polisi.

Habari zaidi zinasema kuwa Muro, ambaye alishinda tuzo ya Mwanahabari Bora wa mwaka 2009 kutokana na habari yake ya rushwa inayofanywa na askari wa usalama barabarani. na taarifa zinaeleza kuwa likamatwa wakati akiwa hoteli ya Sea Cliff.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata, Muro alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na polisi mara baada ya kuarifiwa na mfanyabiashara mmoja, ambaye jina halijawekwa bayana na polisi, kuwa mwandishi huyo amedai rushwa ya Sh10 milioni.

Habari zinadai kuwa mwandishi huyo alikamatwa muda mfupi baada ya kukabidhiwa fedha.

No comments:

Post a Comment